sw_tn/dan/02/36.md

1010 B

Maelezo ya jumla

Danieli anaendelea kuongea na mfalme

Na sasa tutamwambia mfalme

Hapa kiwakilishi "tu" kinamrejelea Danieli peke yake. Inawezekana ametumia muundo wa wingi katika unyenyekevu kuepuka kuchukua heshima kwa kujua maana ya ndoto ambayo Mungu ameifunua kwake.

mfalme wa wafalme

"mfalme wa muhimu sana" au "mfalme anayetawala juu ya wafalme wengine"

nguvu, uweza

Maneno haya kimsingi yanamaanisha kitu kile kile.

Amevitia mkononi mwako

Hapa neno "mkono'' linarejelea utawala. "amekupa utawala"

sehemu ambazo binadamu huishi

sehemu imetumika kuwakilisha watu ambao wanaishi hapo.

Amekupa wanyama wa mwituni na ndege wa angani katika mkono wako,

Hapa neno "mkono" linarejelea utawala. "Amekupa utawala juu ya wanyama wa mwituni na ndege wa angani"

ndege wa angani

hapa neno "angani" limetumika kumaanisha mbinguni.

Wewe u kichwa cha dhahabu cha sanamu

Katika ndoto ya mfalme kichwa cha sanamu kinamwakilisha mfalme. "Kichwa cha dhahabu kinakumaanisha wewe mfalme"