sw_tn/amo/03/01.md

1.9 KiB

neno

"Neno" linarejea kwenye kitu ambacho mtu amesema. Njia tofauti tofauti za kutafsiri neno "neno" au "maneno" inajumuisha, "kufundisha" au "ujumbe" au "habari" au "kusema" au "kilichosemwa." Wakati inamrejelea Yesu kama "Neno," hili neno lingetafsiriwa kama "ujumbe" au "usemi."

Yahwe

Neno "Yahwe" linatokana na jina ambalo alilojifunua wakati alipozungumza na Musa kwenye kichaka kilichokuwa kikiungua. Neno "Yahwe" linatokana na neno linalomaanisha, "kuwa" au "kuishi."

Israeli, Waisraeli, taifa la Israeli

Neno "Israeli" ni jina la Mungu alilokuwa amempa Yakobo. Linamaana, "amepambana na Mungu."

familia

Neno "familia" linarejea kwenye kundi la watu ambao wanauhusiano wa ndugu na kawaida inamuhusisha baba, mama, na watoto. Mara chache inawahusisha ndugu kama vile babu na bibi, wajukuu, wajomba na shangazi. Neno "familia" pia limetumika kurejea kwa watu ambao wanauhusiano kiroho, kama vile watu ambao ni sehemu ya familia ya Mungu kwa sababu wanamwamini Yesu.

Misri, Wamisri

Misri ni nchi katika upande wa kaskazini mwa Afrika, kuelekea kusini mashariki mwa nchi ya Kanaani. Mmisri ni mtu anayetoka nchi ya Misri.

aliyechaguliwa, chagua, watu waliochaguliwa, Aliyechaguliwa, teule

Neno, "mteule" maana halisi "waliochaguliwa" au "watu waliochaguliwa" na inarejea kwa wale ambao Mungu amewateua au kuwachagua kuwa watu wake. "Aliyechaguliwa" au "Aliyechaguliwa na Mungu" ni jina linalomrejea Yesu, ambaye ni Masiha aliyechaguliwa.

adhibu, adhabu

Neno "adhibu" linamaanisha kumsababisha mtu kuteseka kwa matokea hasi kwa kufanya jambo lisilo sahihi. Neno "adhabu" linarejea kwa matokeo hasi ambayo yametolewa kama matokeo ya hiyo tabia mbaya.

dhambi, enye dhambi, mwenye dhambi, kufanya dhambi

Neno "dhambi" linarejea kwa matendo, mawazo, na maneno ambayo ni kinyume na mapenzi ya Mungu na sheria. Dhambia inaweza kurejewa kwa kutokufanya kitu ambacho Mungu anataka tufanye.