sw_tn/act/14/11.md

40 lines
1.3 KiB
Markdown

# alichokifanya Paulo
Hii inamaanisha uponyaji wa Paulo kwa kiwete.
# miungu imeshuka kwetu
Idadi kubwa ya watu iliamini kuwa Paulo na Barnaba walikuwa miungu ya kipagani walioshuka toka mbinguni. "miungu wameshuka toka mbinguni kuja kwetu"
# katika lahaja ya Likaonia
"katika lugha yao ya Kilikaonia" (UDB). Watu wa Listra walizumngumza Kilikaonia na Kigriki pia.
# katika mfano wa mwanadamu
Watu hawa waliamini kuwa miungu walihitaji kubadili mionekano yao ili wawe kama binadamu.
# walimuita Barnaba "Zeu"
Zeu alikuwa mfalme juu ya miungu wengine wote wa kipagani.
# Paulo, Herme, kwa sababu alikuwa msemaji mkuu
Herme alikuwa mungu wa kipagani aliyeleta ujumbe kutoka kwa Zeu na miungu wengine.
# Kuhani wa Zeu, ambaye hekalu lake lilikuwa nje tu ya mji, alileta
Inaweza kusaidia kuweka taarifa ya ziada kuhusu kuhani. "Kulikuwa na hekalu nje tu ya mji ambapo watu walimwabudu Zeu. Kuhani aliyehudumu katika hekalu aliposikia kile ambacho Paulo na Barnaba walichokifanya, alileta
# ng'ombe na mashada ya maua
Ng'ombe walikuwa ni wakutolewa sadaka. Mashada yalikuwa mojawapo kati ya kuwawekea mataji Paulo na barnaba, au kuwawekea ng'ombe kwa ajili ya sadaka.
# milangoni
Milango ya miji mara nyingi ilitumika kama sehemu ya kukutana kwa watu wa mji husika.
# walitaka kutoa sadaka
"walitaka kutoa sadaka kwa Paulo na Barnaba kama miungu Zeu na Herme.