sw_tn/2ti/04/06.md

1.5 KiB

muda wa kuondoka kwangu umewadia

"Karibuni nitakufa na kuiacha dunia hii", Paulo alitambua kuwa hataishi kwa muda mrefu.

Nimeshindana katika mashindano mema

Hii ni michezo mfano wa mapigano, kumenyana, au ndondi. Paul amefanya kwa nguvu zake zote. Hii pia inaweza kutafsiriwa kama "Nimefanya kwa uwezo wote" au "Nilijitoa kwa nguvu zangu zote."

mwendo nimeumaliza

Picha hii inaashiria kumaliza maisha kama kufikia mstari wa kumalizia mbio. "Mimi nimemalize kile ninachohitajika kufanya."

imani nimeilinda

Maana inawezekana ikawa ni 1) "niimezishika mafundisho kuhusu nini tunaamini mbali na kila aina ya upotofu" au 2) "Nimekuwa mwaminifu katika kufanya huduma yangu"

Taji ya haki imewekwa kwa ajili yangu

"nitapewa taji ya haki'

Taji ya haki

Maana inaweze kuwa i 1) taji ni tuzo ambayo Mungu huwapa watu ambao wamekuwa wakiishi kwa njia sahihi au 2) taji ni mfano kwa ajili ya haki. Kama ambavyo hakimu wa mbio inatoa taji kwa mshindi, Paulo atakapomaliza maisha yake, Mungu atamtangaza kwamba Paulo ni mwenye haki.

taji

ni shada iliyotengenezwa kwa majani ya mti (laurel) ambayo ilitolewa kwa washindi wa mashindano ya riadha

siku ile

"siku ambayo Bwana atarudi tena" au "kwa siku ile Mungu atakapo wahukumu watu"

tayari nimekwisha kumiminwa

Paulo anazungumzia utayari wake wa kufa akijifananisha na kikombe cha mvinyo kilivyo tayari kumiminwa kama sadaka kwa Mungu.

bali pia kwa wote wanaongojea kwa shauku kuonekana kwake.

Hii inaweza kuelezewa kama tukio la wakati ujao. "lakini pia atawapa wale wangojao kwa shauku kurudi kwake"