sw_tn/2ti/01/03.md

1.2 KiB

Ninayemtumikia, kama mababa zangu walivyofanya

Paulo alimwabudu Mungu yuleyule ambaye mababu zake walimwabudu. "...ambaye ninafanya majukumu yangu kama Mkristo kama mababu zangu waliokuja kabla yangu walivyofanya"

Kwa nia njema

"kwa nia safi." Hasumbuliwi na fikra za matendo maovu kwa sababu kila mara alijaribu kufanya yaliyo mema.

Ninapowakumbuka ninyi

"Ninapowakumbuka ninyi kila mara" au "ninapowakumbuka kila wakati"

Usiku na

inaweza kuwa na maana 1) "maombi yangu usiku na mchana" au 2) "Ninawakumbuka kila mara usiku na mchana" au 3) "natamani kuwaona usiku na mchana."

Natamani kukuona

"nasubiri sana kukuona"

Nakumbuka machozi yako

"naweka mambo yote yanayokutesa kwenye akili yangu"

Nijawe na furaha

"niwe na furaha sana" au "nifurahie"

Naikumbuka

"kwa sababu nimekuwa nikiikumbuka" au "nilipokuwa nikiikumbuka" au "kwa kuwa naikumbuka"

Imani yako iliyo thabiti

"imani yako ya kweli" au "imani isiyo ya unafiki." inamaanisha kutokuficha kitu au kuwa mkweli.

imani... iliyokuwa kwanza kwa bibi yako... ipo kwako pia

Bibi yake na Timotheo alikuwa mwanamke mcha Mungu, na Paulo anaifananisha imabi ya Timotheo na ya bibi yake.

Loisi ... Yunisi

Haya ni majina ya wanawake.