sw_tn/2ki/25/01.md

964 B

katika mwaka wa tisa

Namba tisa mara nyingi imetumika katika Biblia kueleza nafasi ya kitu kilicho katika orodha.

katika mwezi wa kumi, na siku ya kumi ya mwezi

Huu ni mwezi wa kumi wa kalenda Kiebrania. Siku ya kumi ikaribu na mwishoni mwa mwezi wa kumi na mbili kwenye kalenda za Magharibi. Hiki ni kipindi cha msimu wa baridi wakati huo huweza kuwa na baridi na barafu.

kuja na jeshi lake lote juu ya Yerusalemu

Jina "Yerusalemu" ni ishara kwa ajili ya watu waishio humu. "Kuja na jeshi lake lote kupigana juu ya watu wa Yerusalemu" au "kuja na jeshi lake lote kuishinda Yerusalemu"

siku ya tisa ya mwezi wa nne

Huu ni mwezi wa kalenda ya Kiebrania. Siku ya tisa liyo karibu na mwezi wa Saba kwa kalenda ya Magharibi. Hiki ni kipindi cha majira ya ukame wakati huo huwa na mvua kidogo au hakuna kabisa.

watu wa nchi

Hawa ni wenyeji wa Yerusalemu, pamoja na wakimbizi kutoka vijiji vilivyozunguka waliokimbia Yerusalemu wakati vita ilipoanza.