sw_tn/2ki/03/26.md

913 B

Mfalme Mesha

Tafsri jina la huyu mfalme kama ulivyofanya katika 3:4.

kwamba ameshindwa

"kwamba jeshi lake lilishindwa"

watu hodari wa upanga mia saba

"hodari wa upanga 700"

hodari wa upanga

maaskari ambao hupigana kwa upanga

kuvunja kupita

"lazimisha njia kupita." Kulikuwa na maaskari wengi wakipigana kwenye uwanja wa vita ambao ulifanya kuwa vigumu kuondoka kwenda kwenye umati.

kumtolea kama sadaka ya kuteketezwa

Mfalme Mesha alimteketeza mwanaye kwa moto hadi akafa. Alifanya hivi kama sadaka kwa Kemoshi, mungu wa uongo wa Moabu. Maana kamili ya hii kauli inaweza kuwekwa wazi.

Hivyo kulikuwa na hasira kubwa juu ya Israeli

Hapa neno "hasira" linaweza kuelezwa kama kitenzi. Kuna maana mbili ziwezekanazo kwa yule aliye na hasira hapa 1) Maaskari wa Moabu. "Hivyo maaskari wa Moabu walikuwa na hasira sana na Israeli" au 2) Mungu. "Hivyo Mungu alikuwa na hasira sana na Israeli"