sw_tn/2co/05/06.md

837 B

Sentensi Unganishi

Kwa sababu waamini watakuwa na miili mipya na kuwa na Roho Mtakatifu kama ahadi, Paulo anawakumbusha kuishi kwa imani ili waweze kumfurahisha Bwana. Anaendelea kuwakumbusha kuwavuta na wengine kwa sababu waamini wataonekana katika kiti cha hukumu cha Kristo na kwa sababu ya pendo la Kristo aliyekufa kwa ajili ya waamini.

wakati tuko nyumbani katika mwili

Paulo anazungumza juu ya miili inayoonekana kama vile ilikuwa mahali ambapo mtu hukaa.

tuko mbali na Bwana.

"hatuko nyumbani pamoja na Bwana " au " hatuko mbinguni pamoja na Bwana"

tunatembea kwa imani, sio kwa kuona

"tunaishi kwa imani, na siyo kwa mujibu wa kile tunachokiona"

Ni bora tuwe mbali kutoka kwenye mwili

Hapa neno "mwili" lina maanisha "mwili unaoonekana"

nyumbani pamoja na Bwana.

"nyumbani pamoja na Bwana mbinguni"