sw_tn/2co/03/14.md

1.2 KiB

Lakini fahamu zao zilikuwa zimefungwa

"Lakini mioyo yao ilikuwa migumu." Paulo anazungumza juu ya mioyo ya watu wa Israeli kama kifaa ambacho chaweza kufungwa au kufanywa kigumu. Ufafanuzi huu humaanisha kwamba walikuwa hawawezi kuelewa kile wanacho kiona.

Hata mpaka siku hii

Tungo hizi zinarejea akati ambao Paulo alikuwa akiandika kwa Wakorintho.

utaji uleule bado unabaki juu ya usomaji wa agano la kale

kama ilivyo kwa Waisraeli wasingeweza kuona utukufu juu ya uso wa Musa kwa sababu alifunika uso wake na utaji , kuna utaji wa kiroho unaowazuia watu kutoelewa wanaposema agano la kale.

juu ya usomaji wa agano la kale

"Wakati mtu anaposema agano la kale" au " Wakati wanaposikia mtu fulani anaposoma agano la kale"

Haijawekwa wazi, kwa sababu ni katika Kristo pekee inaondolewa mbali.

Hapa inajumuisha usahihi wa neno "hilo" inarejea "utaji uleule"

wakati wowote Musa asomwapo

Hapa neno " Musa" linarejea kwenye sheria ya agano la kale.

utaji hukaa juu ya mioyo yao

hapa neno "mioyo"linarejea kwenye moyo na mawazo. Utaji wa kiroho hufunika mioyo yao, kuwazuia wasiweze kuelewa agano la kale.

utaji unaondolewa.

Hii ina maanisha kwamba sasa wamepewa uwezo wa kufahamu.