sw_tn/1sa/02/03.md

857 B

Taarifa ya jumla:

Hana anaendelea kumwimbia Bwana wimbo. Anazungumza kama vile watu wengine wanamsikiliza.

Hakuna majivuno

"hakuna maneno ya majivuno"

Kwa yeye matendo hupimwa

Hii inaweza kuandikwa kama "Yeye anapima matendo ya watu"

Pinde za mashujaa zimevunjika

Yaweza kuwa na maana ya 1) pinde zenyewe zimevunjika au 2) watu waliobeba pinde wamekatazwa kufanya. "Watu wenye ushujaa wamenyimwa kufanya"

Pinde za mashujaa zimevunjika

Hii inaweza kutafsiriwa kama "Bwana amezivunja pinde za mashujaa" au "Bwana amewafanya hata watu wenye nguvu kuwa dhaifu"

wale wanaojikwaa hujivika nguvu kama mshipi

Hii inamaanisha kuwa hawatajikwaa tena bali nguvu zao zitakuwa pamoja nao kama mshipi uliobana. "Bali atawafanya waliojikwaa kuwa na nguvu"

kujivika ... mshipi

Hiki ni kitendo cha kuvaa kitu kuzunguka kiuno na kujiandaa na kazi.