sw_tn/1co/16/19.md

1.2 KiB

Kanisa

katika agano jipya neno " kanisa" lina maana ya kundi la watu wanaomwamini Yesu ambao walikutana pamoja kuomba na kusikia mahubiri ya neno la Mungu. Mara nyingi Neno "kanisa" linamaanisha wakristo wote.

Asia

Nyakati za Biblia, "Asia" ilikuwa ni jina mkoa au jimbo katika dola la Warumi. Hii sehemu ilikuwa upande wa magharibi na kwa sasa inajulikana kama nchi ya Utiruki. Miji kama Efeso, na Kolose ilikuwa katika eneo hili la Asia ambapo Paulo alisafiri na kuhubiri injili.

Akila

Akila alikuwa mkristo wa Kiyahudi kutoka katika jimbo la Ponto, mkoa wa kusini mwa pwani ya bahari nyeusi().

Priska

Priska alikuwa mke wa Akila yeye na mume wake walikuwa wakristo waliofanya kazi ya umisheni pamoja na mtume Paulo.

Bwana

Neno" Bwana" linamaana y mtu mwenye kumikili au mamlaka juu ya watu. Neno hili linapoandikwa kwa herufi kubwa humaanisha Mungu.

takatifu

Neno "takatifu" huzungumzia tabia ya Mungu ambayo ni kamilifu na imejitenga mbali na dhambi. ni Mungu pekee ambaye ni mtakatifu, huwa anawafanya watu na vitu kuwa watakatifu

busu

Busu ni tendo la mtu kuweka mdomo wake kwenye mdomo wa mtu mwingine. Katika Biblia neno hili busu wakati mwingine limetumika kumaanisha kuagana au kuwambia mtu kwahari.