sw_tn/1co/15/31.md

1.1 KiB

Nakufa kila siku. Hili nalisema kwa kujisifu kwa ajili yenu

" ninajisifu kwa ajili yenu, hivyo kila mmoja anajua kwamba nasema ninaposema ninakufa kila siku"

Ninakufa kila siku.

Paulo anacho maanisha hapa ni (1)kila siku najipambanua kwa kifo cha Kristo kwa kufisha tamaa mbaya ndani yake 2) kila siku aliishi akijua kuwa kuna watu walikuwa wakitafuta kumuua.

Inanifaidia nini..nilipigana na wanyama wakali huko Efeso... hawafufuliwi?

Paulo anataka Wakorintho wafahamu jambo hilo hata bila kuwaambia. kwa maneno mengine anasema " sikupata chochote...kwa kupigana na wanyama huko Efeso... hawafufuliwi"

kama nilipigana na wanyama katika Efeso

Kuna uwezekano maana ni 1) Paulo alikuwa anaongea kwa mfano kuhusu hoja yake na wapagani waliosoma au mafarakano mbalimbali na watu waliotaka kumuua au 2) Anathibitisha kwamba aliwahi kuwekwa kwenye uwanja kupambana dhidi ya wanyama hatari.

Na tule na kunywa, kwa kuwa kesho tunakufa.

Paulo anahitimisha kwamba kama hakuna maisha mengine baada ya kifo, ni bora kwetu kuyafurahia maisha haya kwa kadri tuwezavyo, kwa kuwa kesho maisha yetu yataisha bila matumaini yoyote