sw_tn/1ch/21/09.md

2.2 KiB

Yahweh

Neno "Yahweh" ni jina binafsi la Mungu ambalo alilidhihirisha alipokuwa anazungumza na Musa kwenye kichaka cha moto.

  • Jina "Yahweh" limetokana na neno linye maana, "Kuwa" au "kuwepo."
  • Maana inayowezekana kuwa ya "Yahweh" inajumuisha, "ndiye" au "Ndimi" au "anaye sababisha kuwa."
  • Jina hili linadhihirisha kuwa Mungu anaishi na ataendelea kuishi milele. pia linamaanisha yupo siku zote.
  • Kufuata mila, tafsiri nyingi za Biblia zinatumia neno "BWANA" kuwakilisha "Yahweh." Mila hii ni matokeo ya ukweli kihistoria, kwamba watu wa Kiyahudi walikuwa na uwoga wa kutamka jina Yahweh na kuanza kusema "Bwana" kila muda neno "Yahweh" lilitokea katika nakala. Biblia za kisasa zimeandika "BWANA" kwa herufi kubwa zote kuonesha heshima kwa jina la Mungu binafsi na kulitofautisha na "Bwana" ambalo na tofauti na neno la Kiebrania.
  • Neno "Yahweh" halitokei kamwe katika nakala halisi ya agano jipya; neno pekee la kiyahudi la "Bwana" ndo linalotumika, hata kwenye nukuu za agano la kale.

Gadi

Gadi ni moja ya wana wa Yakobo, ambaye ni, Israeli.

  • Familia ya Gadi ilikuwa moja ya makabila kumi na mbili ya Israeli.
  • Mwanamume mwingine katika Biblia aliye itwa Gadi alikuwa nabii aliye mkabili Daudi kwa dhambi yake ya kuchukuwa takwimu ya watu Waisraeli.
  • Miji, Baaligadi na Migdalidadi yote ni maneno mawili katika nakala halisi na wakati mwengine uandikwa, "Baali Gadi" na "Migdali Gadi."

nabii, unabii, kutoa unabii, muonaji, nabii wa kike

"nabii" ni mwanaume anaye ongea jumbe za Mungu kwa watu. Mwanamke anaye fanya haya anaitwa "nabii wa kike"

  • Mara nyingi manabii waliwaonya watu wa geuke toka dhambi zao na kumtii Mungu.
  • "unabii" ni ujumbe nabii anauzungumza. "Kutoa unabii" ni kuzungumza jumbe za Mungu.
  • Mara nyingi ujumbe wa unabii ulikuwa kuhusu jambo litakalo tokea mbeleni.
  • Unabii nyingi katika Agano la Kale zimeshatimia.
  • Katika Biblia mkusanyiko wa vitabu vilivyo andikwa na manabii wakati mwingine vinatajwa kama "manabii"
  • Kwa mfano, maneno, "sheria na manabii" ni namna ya kutaja maandiko yote ya Kiebrania, ambayo yanajulikana kama "Agano la Kale"
  • Jina la kale la nabii lilikuwa "muonaji" au "mtu anaye ona"
  • Wakati mwengine neno "muonaji" la husu nabii wa uongo au mtu anaye tumia uganga.