sw_tn/act/13/28.md

24 lines
599 B
Markdown
Raw Normal View History

2018-04-12 01:01:04 +00:00
# Maelezo ya jumla
Viwakilishi vya majina, vinawakilisha Wayahudi na Viongozi wa dini zao katika Yerusalemu.
# hawakupata sababu nzuri kwa kifo ndani yake
"Hawakupata sababu zenye maana kwanini Yesu alipaswa auawe"
# Walimwomba Pilato amwue
Neno "Kumwomba" ni neno lenye nguvu likimaanisha "Kutaka, kulazimisha, kudai"
# Walipomaliza mambo yote yaliyoandikwa kuhusu yeye
"Wakati walipomtendea Yesu, kila kitu walichokuwa wamekisema manabii kilitimia.
# walimshusha kutoka mtini
"Walimwua Yesu na kuuondoa mwili wake kutoka kwenye msalaba baada ya kufa."
# kutoka mtini
"Kutoka msalabani"