Tafsiri zingine zimetenga mistari ya ushairi mbele zaidi kuelekea kulia kuliko maandishi mengine ili yasomeke kwa urahisi. ULB hufanya hivi na ushairi ambao umenukuliwa kutoka Agano la kale katika 4:18
Aya hii inatumia neno "Watu wa mataifa" kumaanisha watu wote wasiomcha Mungu na siyo Wayahudi. Haiwajumuishi Watu wa mataifa ambao wameisha kuwa Wakristo. Zambi za tamaa na ulevi na kuabudu sanamu zilikua tabia ya wasiomcha Mungu.
Petero anatumia vifungu hivi vya maneno kuwaeleza wasomaji wake anachotaka wafanye. Ni kama maagizo ya kiamri kwa sababu anataka wasomaje wake wayatii. Lakini ni kama anamwambia mtu mmoja anachotaka na watu wengine wanaambiwa cha kufanya.