forked from WA-Catalog/sw_tn
32 lines
1.2 KiB
Markdown
32 lines
1.2 KiB
Markdown
|
# Taarifa ya jumla:
|
||
|
|
||
|
Mwandishi anaendelea kuwaelezea watu wanaoamini kuwa mali yao itawaokoa.
|
||
|
|
||
|
# Kama kondoo
|
||
|
|
||
|
Mwandishi anawafananisha watu watakaokufa kama kundi la kondoo. Kama kondoo amabvyo hawawezi kutoroka wakati bucha anapoamua kuwachinja, kwa hiyo watu hawatatoroka ukifika wakati wao kufa.
|
||
|
|
||
|
# wamechaguliwa
|
||
|
|
||
|
"Mungu amewachagulia"
|
||
|
|
||
|
# mauti itakuwa mchungaji wao
|
||
|
|
||
|
Mwandishi anazungumzia watu kufa kwa kutaja mauti kama mtu ambaye ni mchungaji anayewaongoza katika kaburi. "mauti itawapeleka kama mchungaji anavyowaongoza kondoo kwenda machinjioni"
|
||
|
|
||
|
# asubuhi
|
||
|
|
||
|
Hapa neno "asubuhi" ni sitiari inayomaanisha wakati ambapo Mungu atawathibitisha watu wenye haki na kuwaokoa kutoka kwa watu waovu.
|
||
|
|
||
|
# miili yao itamezwa kuzimu
|
||
|
|
||
|
Mwandishi anazungumzia kuzimu, sehemu ya wafu, kana kwamba ni mtu au mnyama. Anazungumzia uozo wa miili iliyokufa kana kwamba kuzimu inaila. "miili yao itaoza kaburini"
|
||
|
|
||
|
# Mungu atakomboa maisha yangu kutoka kwenye nguvu ya kuzima
|
||
|
|
||
|
Mwandishi anazungumzia kuzimu kana kwamba ni mtu aliye na nguvu juu ya wale walio kufa. Kutokana na muktadha, inadokezwa kwamba uwezo huu unamaanisha kuteketeza miili ya wafu.
|
||
|
|
||
|
# Mungu atakomboa maisha yangu
|
||
|
|
||
|
Hapa neno "maisha" linamaanisha mtu mzima. "Mungu atanikomboa"
|