sw_tn/psa/069/013.md

45 lines
1.3 KiB
Markdown
Raw Normal View History

2019-05-21 20:17:16 +00:00
# katika muda utakaokubali
"katika muda wako uliokubalika" au "utakapokuwa tayari"
# nijibu katika uaminifu wa wokovu wako
"niokoe kwa sababu unanipenda kwa uaminifu, kama ulivyoahidi kufanya"
# Nivute nje ... usiniache nizame
Misemo hii miwili ina maana moja.
# Nivute nje ya matope, na usiniache nizame
Mwandishi anazungumzia hatari yake kutoka kwa adui zake kana kwamba alikuwa akizama katika shimo la matope. "Usiniruhusu niendelee kuzama katika matope"
# acha nichukuliwe
Hapa "kuchukuliwa" inamaanisha kutolewa kutoka hatarini. "nitoe" au "niokoe"
# niokolewe kutoka
"tafadhali niokoe kutoka"
# maji marefu ... mafuriko ya maji ... kilindi
Misemo hii ina maana moja.
# niokoa kutoka kwenye maji marefu
Mwandishi anazungumzia hatari yake kutoka kwa adui zake kana kwamba anazama katika maji marefu.
# mafuriko ya maji yamenilemea
Mwandishi anazungumzia hatari yake kutoka kwa adui zake kana kwamba mafuriko ya maji yalikuwa yakimfunika kabisa.
# kilindi kinanimeza
Mwandishi anazungumzia kilindi kana kwamba ni mnyama hatari aliyekuwa tayari kumla. "maji marefu yananimeza kama mnyama hatari"
# Usiruhusu shimo lifunge mdomo wake kwangu
Hapa "shimo" linazungumziwa kana kwamba lina mdomo kama mtu na linaweza kumla mwandishi. "Usiruhusu shimo linimeze" au "Usiache shimo la mauti lifunge juu yangu"