# katika muda utakaokubali "katika muda wako uliokubalika" au "utakapokuwa tayari" # nijibu katika uaminifu wa wokovu wako "niokoe kwa sababu unanipenda kwa uaminifu, kama ulivyoahidi kufanya" # Nivute nje ... usiniache nizame Misemo hii miwili ina maana moja. # Nivute nje ya matope, na usiniache nizame Mwandishi anazungumzia hatari yake kutoka kwa adui zake kana kwamba alikuwa akizama katika shimo la matope. "Usiniruhusu niendelee kuzama katika matope" # acha nichukuliwe Hapa "kuchukuliwa" inamaanisha kutolewa kutoka hatarini. "nitoe" au "niokoe" # niokolewe kutoka "tafadhali niokoe kutoka" # maji marefu ... mafuriko ya maji ... kilindi Misemo hii ina maana moja. # niokoa kutoka kwenye maji marefu Mwandishi anazungumzia hatari yake kutoka kwa adui zake kana kwamba anazama katika maji marefu. # mafuriko ya maji yamenilemea Mwandishi anazungumzia hatari yake kutoka kwa adui zake kana kwamba mafuriko ya maji yalikuwa yakimfunika kabisa. # kilindi kinanimeza Mwandishi anazungumzia kilindi kana kwamba ni mnyama hatari aliyekuwa tayari kumla. "maji marefu yananimeza kama mnyama hatari" # Usiruhusu shimo lifunge mdomo wake kwangu Hapa "shimo" linazungumziwa kana kwamba lina mdomo kama mtu na linaweza kumla mwandishi. "Usiruhusu shimo linimeze" au "Usiache shimo la mauti lifunge juu yangu"