sw_tn/luk/22/01.md

29 lines
1.0 KiB
Markdown
Raw Normal View History

2018-04-12 01:01:04 +00:00
# Maelezo ya ujumla:
Hii ni sehemu inayofuata ya simulizi. Yuda anakubali kumsaliti Yesu. Mistari hii inatupa taarifa za msingi kuhusu sehemu hii ya simulizi.
# Basi
Neno hili linatumika hapa sehemu mpya ya simulizi
# sikukuu ya mkate usiyotiwa chachu
sikukuu hii ilikuwa inaitwa kwa jina hili kwa sababu wakati wa sikukuu, Wayahudi hawakula mkate ambao ulikuwa umetengenezwa na chachu. Tafsiri mbadala: "Sikukuu ambapo wangekula mkate usiyotiwa chachu"
# Mkate usiyotiwa chachu
Huu ni mkate ambao hauna chachu au hamila ili kuufanya uumuke. Tafsiri mbadala: "Mkate bila Hamila."
# ilikuwa imekaribia
"ilikuwa tayari sana kuanza"
# namna ya kumuua Yesu
Makuhani na waandishi hawakuwa na mamlaka ya kumuua Yesu wao wenyewe, lakini walitegemea kupata watu wengine wa kumuua. Tafsiri mbadala: "Namna gani ambavyo wangesababisha Yesu kuuwawa" au "namna ambavyo wangesababisha mtu amuuwe Yesu."
# waliwaogopa watu
Inaweza kutafsiriwa kama 1) "walikuwa na wasiwasi wa kile ambacho watu wangefanya" au 2) "walikuwa na wasiwasi kwamba watu wangemfanya Yesu mfalme."