sw_tn/zec/09/11.md

28 lines
745 B
Markdown
Raw Permalink Normal View History

2019-05-21 20:17:16 +00:00
# Lakini kwenu
Hapa "ninyi" inamaanisha watu wa Israeli.
# shimo ambalo halina maji
Shimo hapa linawakilisha uhamisho.
# Rudini ngomeni
"Rudini katika nchi yenu mahali mtakapokuwa salama"
# wafungwa wa tumani
Hii inamaanisha Waisraeli waliokuwa kifungoni waliokuwa bado wanamatumaini kwamba Mungu atawakomboa.
# pinda Yuda kama upinde wangu
Watu wa Yuda wanatajwa kama walikuwa upinde uliobebwa na Mungu kwa vita.
# kulijaza podo langu kwa Efraimu
Watu wa Israeli, ufalme wa kaskazini, wanatajwa kama walikuwa mishale ambayo Mungu angewapigia adui zake. Podo ni mfuko unaotunza mishale ya askari.
# Nimewainua wana wenu, Sayuni, kinyume cha wana wenu, Ugiriki,
Mungu anazungumza na watu wa mataifa mawili tofauti kwa wakati mmoja.