sw_tn/rom/08/09.md

28 lines
1.1 KiB
Markdown
Raw Permalink Normal View History

2018-04-12 01:01:04 +00:00
# katika mwili...katika Roho
Angalia maneno haya yalivyotafsiriwa hapo awali.
# Roho...Roho wa Mungu...Roho wa Kristo
Haya yote yanamuelezea Roho Mtakatifu
# kama ni kweli kwamba
Maneno haya hayamaanishi kwamba Paulo ana mashaka kwamba baadhi ya watu hawana Roho wa Mungu. Paulo anataka wote watambue kwamba wanaye Roho wa Mungu.
# Kama Kristo yumo ndani yenu
Jinsi Kristo anavyoishi ndani ya mtu inaweza kuwekwa wazi. "Kama Kristo anaishi ndani yako kupitia Roho Mtakatifu"
# kwa upande mwingine, mwili umekufa kwa mambo ya dhambi, lakini kwa upande mwingine
Kipande cha sentensi "kwa upande mwingine" na "lakini kwa upande mwingine" huonesha njia mbili za namna ya kufikiri kuhusu jambo fulani. "mwili umekufa katika mambo ya dhambi, lakini"
# mwili umekufa kwa mambo ya dhambi
Uwezekano wa maana hizi mwili 1) mtu amekufa kiroho katika nguvu ya dhambi au 2) bado mwili wa nyama utakufa kwasababu ya dhambi.
# roho ipo hai kwa mambo ya haki
maana yake yaweza kuwa 1) mtu yupo hai kiroho, Mungu amempa nguvu kufanya yaliyo sahihi au 2) Mungu atamrejesha mtu uzimani baada ya kufa kwasababu Mungu ni mwenye haki na huwapa walioamini uzima wa milele.