sw_tn/rom/01/01.md

28 lines
1.0 KiB
Markdown
Raw Permalink Normal View History

2018-04-12 01:01:04 +00:00
# Paulo
Lugha yako inaweza kuwa na namna ya kumtambulisha mwandishi wa barua. "Mimi Paulo naandika barua hii." Unaweza pia kusema ni kwa nani barua iliandikwa.
# kuitwa kuwa mtume, na kutengwa kwa ajili ya injili ya Mungu
"Mungu alinita mimi kuwa mtume na alinichagua kuwaambia watukuhusu injili"
# Kuitwa
Hapa inamaana kuwa Mungu aliteua au kuchagua watu kuwa watoto wake, kuwa watumishi wake na watangazaji wa ujumbe wake wa wokovu kupitia kwa Yesu.
# Hii ni injili ambayo aliiahidi kabla kwa mitume wake kwenye maandiko matakatifu
Mungu aliwaahidi watu wakekwamba atawaandalia ufalme. Aliwaambia mitume waandike ahadi hizi kwenye maandiko.
# Ni kuhusu mwana wake
Hii inamaanisha "Injili ya Mungu," habari njema ambayo Mungu aliwaahidi kuwapa mwanawe ulimwenguni.
# Mwana
Hiki ni cheo cha muhimu sana kwa Yesu, Mwana wa Mungu.
# Aliyezaliwa toka kwa uzao wa Daudi kutokana na mwili
Hapa neno "mwili" linamaanisha mwili unaoonekana. "Ambaye ni uzao wa Daudi kutokana na asili ya mwili" au "aliyezaliwa kwenye familia ya Daudi."