sw_tn/rev/03/14.md

24 lines
850 B
Markdown
Raw Permalink Normal View History

2018-04-12 01:01:04 +00:00
# Taarifa ya Jumla:
Huu ni ujumbe wa Mwana wa Adamu kwa malaika wa kanisa la Laodikia.
# Maneno yake aliye Amina
Hape "aliye Amina" ni jina la Yesu Kristo. Athibitisha ahadi za Mungu kwa kusema amina.
# mtawala juu ya uumbaji wa Mungu
Maana zinazowezekana ni 1)"yule ambaye antawala vitu vyote vilivyoumbwa na Mungu" au 2)"yule ambaye Mungu aliumba vitu vyote kupitia kwake."
# wewe si baridi wala moto
"Baridi" na "moto" inaonesha kuvutiwa kwa mambo ya kiroho au kumpenda Mungu kwa pande mbili tofauti kabisa. Kuwa "baridi" ni kuwa kinyume kabisa na Mungu na kuwa wa "moto" ni kuwa na uchu wa kumtumikia.
# vuguvugu
"joto kidogo." Hii humuelezea mtu aliye na hamu ndogo ya mambo ya kiroho.
# nitakutapika utoke kinywani mwangu
Kuwakataa inazungumziwa kama kuwatapika kutoka kinywani. "Nitawakataa kama vile nitemavyo maji ya uvuguvugu."