sw_tn/rev/01/14.md

36 lines
1.3 KiB
Markdown
Raw Permalink Normal View History

2018-04-12 01:01:04 +00:00
# Kichwa chake na nywele zake zilikuwa nyeupe kama sufu nyeupe kama theluji
Sufu na theluji ni mifano ya vitu ambavyo ni viupe sana. Kurudiwa kwa "nyeupe kama" huonesha msisitizi kuwa zilikua nyeupe mno.
# sufu
Haya na manyoya ya kondoo au mbuzi. Zilikua zinajulikana kuwa nyeupe mno.
# macho yake yalikuwa kama mwali wa moto
Macho yake yanaelezwa kuwa na mwanga kama mwali wa moto. "macho yake yaling'ara kama mwali wa moto"
# Nyayo zake zilikuwa kama shaba iliyosuguliwa sana
Shaba hung'arishwa kuifanya ingae na kurudisha mwanga. "Miguu yake iling'ara sana kama shaba iliyosuguliwa"
# kama shaba iliyosuguliwa sana, kama shaba ambayo imekwisha pitishwa katika moto
Shaba ilisafishwa kwanza kisha kusuguliwa. "Kama shaba iliyosafishwa kwenye tanuu la moto na kusuguliwa"
# tanuu
chombo imara kwa ajili ya kutunzia moto mkali sana. watu huweka vyuma ndani yake na ule moto huunguza takataka zote zilizomo katika chuma.
# sauti ya maji mengi yanayotiririka kwa kasi
Hii ina sauti kuu sana kama sauti ya mto mkubwa unaotiririka kwa kasi, maporomoko ya maji, au ya mawimbi yenye sauti kali baharini.
# kinywani mwake kulikuwa na upanga mkali
Ubapa wa upanga ulikuwa unchomoza kinywani mwake. Upanga wenyewe haukua ukisogea.
# upanga mkali wenye makali kuwili
Hii humaanisha upanga wenye makali mawili, ambao umechongeka pande zote ili kukata pande zote.