sw_tn/rev/01/04.md

48 lines
1.4 KiB
Markdown
Raw Permalink Normal View History

2018-04-12 01:01:04 +00:00
# Taarifa ya Jumla:
Huu ni mwanzo wa barua ya Yohana. Hapa ajitaja kama mwandishi na kuwasalimu watu anaowaandikia.
# neema iwe kwenu na amani kutoka kwake aliyepo...na kutoka kwa roho saba...na kutoka kwa Yesu Kristo
Haya ni matamanio au baraka. Yohana anazungumza kana kwamba hivi ni vitu ambavyo Mungu anaweza kugawa, ingawa ni njia ambazo anatumaini Mungu atawatendea watu wake. "Yule aliyepo...na roho saba...na Yesu Kristo awatendee kwa huruma na kuwawezesha kuishi kwa amani na usalama."
# Kutoka kwake aliyepo
"kutoka kwa Mungu, aliyepo"
# Atakayekuja
Atakayekuwapo baadaye ananenwa kama anayekuja.
# roho saba
Namba saba ni alama ya ukamilifu na utimilifu. "Roho saba" humaanisha mojawapo kati ya Roho ya Mungu au roho saba zinazomtumikia Mungu.
# Mzaliwa wa kwanza wa waliokufa
"mtu wa kwanza kufufuliwa kutoka mautini"
# ametuweka huru
"ametukomboa"
# ametufanya kuwa ufalme, makuhani
"ametuweka kando na kuanza kututawala na kutufanya makuhani"
# Mungu na Baba yake
Huyu ni mtu mmoja. "Mungu na Baba yake"
# Baba
Hili ni jina muhimu la Mungu linaloeleza uhusiano kati ya Mungu na Yesu.
# kwake kuwa utukufu na nguvu
Haya ni matamanio au baraka. Maana zinazowezekana ni 1)"Watu waheshimu utukufu wake na nguvu" au 2) "awe na utukufu na nguvu". Yohana anaomba kwamba Yesu Kristo ataheshimiwa na ataweza kutawala kabisa juu ya kila mtu na kila kitu.
# nguvu
hii inaweza kumaanisha mamlaka yake kama mfalme.