sw_tn/psa/090/003.md

28 lines
903 B
Markdown
Raw Permalink Normal View History

2019-05-21 20:17:16 +00:00
# Unamrudisha mtu mavumbini
Hii inadokezwa kuwa kama jinsi Mungu alivyoumba binadamu wa kwanza, Adamu, kutoka mavumbini, Mungu atasababisha miili ya watu kurudi mavumbini baada ya kufa. "Unawarudisha watu kwenye mavumbi wanapokufa"
# Unamrudisha mtu
Hapa "mtu" inamaanisha watu kwa ujumla.
# Rudini, nyie uzao
"Rudini mavumbini, nyie uzao" au "Rudini kwenye mchanga, nyie uzao"
# nyie uzao wa wanadamu
Hii ni njia ya kumaanisha watu kwa ujumla. "nyie wanadamu" au "nyie watu"
# Kwa kuwa miaka elfu moja machoni pako ni kama siku ya jana inavyopita, na kama kesha la usiku
Mwandishi anamaanisha kuwa kipindi kirefu cha muda kinaonekana kama kipindi kifupi kwa Mungu. "Unaona miaka elfu moja sawa na siku moja ya nyuma, au kama masaa machache ya usiku" au "Hata miaka elfu moja sio muda mrefu kwako"
# miaka elfu moja
"miaka 1,000"
# machoni pako
Hapa "machoni" inawakilisha mawazo. "kwako"