# Unamrudisha mtu mavumbini Hii inadokezwa kuwa kama jinsi Mungu alivyoumba binadamu wa kwanza, Adamu, kutoka mavumbini, Mungu atasababisha miili ya watu kurudi mavumbini baada ya kufa. "Unawarudisha watu kwenye mavumbi wanapokufa" # Unamrudisha mtu Hapa "mtu" inamaanisha watu kwa ujumla. # Rudini, nyie uzao "Rudini mavumbini, nyie uzao" au "Rudini kwenye mchanga, nyie uzao" # nyie uzao wa wanadamu Hii ni njia ya kumaanisha watu kwa ujumla. "nyie wanadamu" au "nyie watu" # Kwa kuwa miaka elfu moja machoni pako ni kama siku ya jana inavyopita, na kama kesha la usiku Mwandishi anamaanisha kuwa kipindi kirefu cha muda kinaonekana kama kipindi kifupi kwa Mungu. "Unaona miaka elfu moja sawa na siku moja ya nyuma, au kama masaa machache ya usiku" au "Hata miaka elfu moja sio muda mrefu kwako" # miaka elfu moja "miaka 1,000" # machoni pako Hapa "machoni" inawakilisha mawazo. "kwako"