sw_tn/psa/042/001.md

28 lines
784 B
Markdown
Raw Permalink Normal View History

2019-05-21 20:17:16 +00:00
# Taarifa ya Jumla:
Usambamba ni kawaida katika mashairi ya Kiebrania.
# Kwa mwanamuziki mkuu
"Hii ni kwa kiongozi wa muziki kutumia katika kuabudu"
# Maschili
Hii inaweza kumaanisha mtindo wa muziki.
# Kama mbawala anavyotweta kwa ajili ya kijito cha maji, vivyo hivyo ninakiua na wewe , Mungu
Mwandishi analinganisha shauku yake kwa ajili ya Mungu na shauku ya mbawala kwa ajili ya maji.
# anavyotweta
kupumua kwa nguvu kutoka kwa mnyama au mtu aliyechoka sana au mwenye kiu
# ninakiua na wewe , Mungu ... Ninakiu na Mungu
Mwandishi anazungumzia hamu yake kubwa kwa ajili ya Mungu kana kwamba ni kiu kikali kwa ajili ya maji.
# nitakuja lini nakutokea mbele za Mungu?
Mwandishi haulizi swali hili ili kupata jibu bali kuonesha shauku yake kubwa ya kuwa mbele za Mungu.