sw_tn/psa/007/006.md

28 lines
957 B
Markdown
Raw Permalink Normal View History

2019-05-21 20:17:16 +00:00
# Inuka, Yahwe, katika hasira yako
Kuinuka inamaanisha kufanya jambo au kuchukua hatua. "Fanya jambo katika hasira yako" au "Wakasirikie adui zangu na uchukue hatua"
# simama dhidi ya gadhabu ya adui zangu
Kupambana na watu kunazungumziwa kama kusimama dhidi yao. "pambana dhidi ya gadhabu ya adui zangu" au "shambulia adui zangu wenye gadhabu juu yangu"
# gadhabu ya adui zangu
Gadhabu yao inaashiria mashambulizi yao. "mashambulizi ya adui zangu" au "adui zangu wanaonishambulia"
# amka
Kuamka kunaashiria kuanza kufanya jambo au kuchukua hatua. "Chukua hatua" au "Fanya kitu"
# kwa ajili yangu
"kunisaidia"
# Mataifa yamekusanyika
Hapa neno "mataifa" linamaanisha majeshi yote yaliokusanyika kushambulia.
# chukua tena nafasi yako unayostahili juu yao
Kutawala watu kunazungumziwa kama kuwa juu yao. Sehemu anayostahili Yahwe inamaanisha mojawapo kati ya mbinguni au kutawala kwa ujumla. "Tawala juu yao kutoka mbinguni" au "Tawala juu yao"