sw_tn/php/01/22.md

16 lines
982 B
Markdown
Raw Permalink Normal View History

2018-04-12 01:01:04 +00:00
# kama kuishi katika mwili huleta tunda katika kazi yangu
Neno "tunda" hapa limetumika kurejelea matokeo mazuri ya kazi ya Paulo. " kama kuishi katika mwili kuna nipa fursa ya kuwatia moyo watu ili waamini katika Kristo."
# inamaana kwamba matunda ya kazi yangu
Neno "tunda" hapa linarejea matokeo mazuri ya kazi ya Paulo. "inamaana kwamba nitaweza kufanya kazi na kazi yangu itazaa matokeo mazuri" au "maana nitakuwa na nafasi zaidi kuwatia moyo watu kumwamini Kristo"
# Ninasukumwa katika vitu viwili
Paulo anazungumzia vile ilivo vigumu kwake kuchagua kati ya kuishi na kufa kama vitu vizito vnavyopingana, kama mawe au magogo, vilikuwa vikimsukuma kwenda kinyume katika wakati mmoja. Lugha yako inaweza kupendelea kupinga kuvuta kuliko kusukuma. "nipo ndani ya mvutano. Sijui kama naweza kuchagua kuishi au kufa"
# Ninahamu ya kuuacha mwili na kuwa na Kristo
Paulo anatumia tafsida hapa kuonyesha kwamba haogopi kufa. "ningependa kufa kwa sababu nitaenda kuwa na Kristo"