sw_tn/mat/10/26.md

32 lines
1.5 KiB
Markdown
Raw Permalink Normal View History

2018-04-12 01:01:04 +00:00
# Sentensi unganishi
Yesu anaendelea kuwaelekeza wanafunzi wake kuhusu dhiki wanayopaswa kuivumilia wakati watakapoenda kuhubiri.
# msiwahofu wao
Hapa "wao" inamaanisha watu wanaowatenda vibaya wafuasi wa Yesu
# hakuna jambo ambalo halitafunuliwa, na hakuna lililojifichwa ambalo halitajulikana
Hizi sentensi zote mbili zinamaanisha kitu kilekile. Yesu anasisitiza kuwa Mungu atayafichua mabo yote. Hii inaweza kutafasiriwa katika mafumo tendaji. "Mungu atafunua mambo ambayo watu wanayaficha."
# Kile ninachowaambia gizani, mkiseme nuruni, na mnachokisikia kwa ulaini masikioni, mkitangaze mkiwa juu ya nyumba
Sentensi zote hizi mbili zinamanisha kitu kilekile. Yesu anasisitiza kuwa wanafunzi wanapaswa kumwambia kila mmoja kile anachowaambia wanafunzi sirini. "Waambie watu mchana kile ninachokuambia gizani, na tangazeni mkiwa juu ya nyumba kile mnchosikia kwenye masikio yenu"
# Kile ninachokuambia gizani
Hapa "giza" linamaanisha "sirini" Ninachowaambia kisirisiri" au "mambo ninayowaambia peke yenu"
# kile ninachokisema nuruni
Hapa neno :nuruni" linamaanisha "kwa uwazi. "Semeni kwa uwazi" au "semeni katika umma"
# Kile mnachokisikia kwa ulaini masikioni mwenu
Hii ni namna ya kusema kunakomaanisha kunong'ona. "Kile ninachowanong'onezea"
# mkitangaze mkiwa juu ya nyumba
mapaa ya nyumba wakati wa Yesu yalikuwa ya bapa, hata watu wali mbali wangeweza kumsikia mtu anapokuwa anaongea kwa sauti ya juu. Hapa mapaa ya nyumba yanamaanisha mahali popote ambapo watu wanaweza kusikia. "Ongea kwa sauti katika eneo la umma ili watu wote wasikie"