sw_tn/mat/05/27.md

32 lines
1.2 KiB
Markdown
Raw Permalink Normal View History

2018-04-12 01:01:04 +00:00
# Sentensi unganishi
Yesu anaendelea kufundisha juu ya jinsi alivyokuja kuitimiliza sheria ya Agano la Kale. Na hapa anaongelea uzinzi na kutamani mwanamke.
# Maelezo kwa ujumla
Yesu anaongea na makutano juu ya kile kinachoweza kutokea katika maisha ya mtu binafsi. Neno "mme..." kutokana na "mmesikia" na "nawaambieni" yametumika katika wingi. Amri ya "Usizini" imetumika katika umoja "usi," lakini unaweza kuitafsiri katika wingi "msi".
# imenenwa kuwa
Hii inaweza kuelezeka katika muundo tendaji. "kuwa Mungu alisema".
# fanya (uzinzi)
Hili neno ni kitenzi kikuu cha kufanya jambo fulani
# Lakini nawaambieni
Neno "nawa" ni msisitizo. Hii inamaanisha kuwa kile ambacho Yesu anasema kina umhimu sawa na kile kilicho kwenye amri kuu kotoka kwa Mungu. Tafsiri kirai hiki katika namna ambayo inaonesha msisitizo huo. Tazama ilivyotafsiriwa katika 5:21
# yeyote amtazamaye mwanamke kwa kumtamani amekwisha kuzini naye moyoni mwake.
Sitiari hii inamaanisha kuwa mwanamume amtamaniye mwanamke anahatia sawa na mwanamume aliyefanya uzinzi halisi.
# amtazamaye mwanamke kwa kumtamani
"na kumtamani mwanamke" au "na kutamani kulala naye"
# moyoni mwake
Hapa "moyo" inamaanisha fikra za mtu. "akilini mwake" au "Katika fikra zake"