sw_tn/mat/03/07.md

32 lines
1.4 KiB
Markdown
Raw Permalink Normal View History

2018-04-12 01:01:04 +00:00
# Taarifa kwa ujumla:
Yohana Mbatizaji aanza kuwakemea Mafarisayo na Masadukayo.
# Enyi uzao wa nyoka wa sumu
Hii ni sitiari. Nyoka wa sumu ni hatari na wanwaklisha uovu. "Enyi nyoka wa sumu waovu!" au "Mu waovu kama nyoka wa sumu."
# nani kawaonya kuikimbia ghadhabu ambayo inakuja
Yohana anatumia swali kuwaonya Mafarisayo na Masadukayo kwa sababu walikuwa wakimwomba kuwabatiza ili kwamba Mungu asiwahukumu, lakini hawakutaka kuacha kufanys dhambi. "hamwezi kuikimbia ghadhabu ya Mungu namna hii" au "msifikiri kwamba mnaweza kuikimbia ghadhabu ya Mungu kwa sababu ya kuwabatiza tu.
# Ikimbieni gadhabu inayokuja
Neno "ghadhabu" linatumika kumaanisha adhabu ya Mungu kwa sababu ghadhabu yake hutangulia. "kimbieni kutoka kwenye hukumu ambayo inakuja" au "iepukeni kwa sababu Mungu anaenda kuwaadhibu ninyi."
# Zaeni matunda yastahiliyo toba
Kirai "zaeni matunda" ni sitiari inayomaanisha matendo ya mtu. "Acha matendo yenu yaoneshe kwamba mmetubu kweli."
# Tunaye Ibrahimu baba yetu
"Ibrahimu ni babu yetu" au "ni wazaliwa wa Ibrahimu." Viongozi wa Kiyahudi walifikiri kwamba Mungu hangewahukumu kwa kuwa ni wazaliwa wa Ibrahimu.
# Kwa maana nawambieni
Hii inaongeza msisitizo kwa kile Yohana anchokwenda kukisema
# Mungu anaweza kumwinulia Ibrahimu watoto hata kutokana na mawe haya.
"Mungu angeweza kufanya wazaliwa wa mwili kutokana hata na mawe haya na kumpa Ibrahimu"