sw_tn/job/02/03.md

28 lines
980 B
Markdown
Raw Permalink Normal View History

2019-05-21 20:17:16 +00:00
# Habari za Jumla:
Mistari hii ipo sawa na 1: 6, isipokuwa kwa ongezeko la "Yeye anashikamana na utimilifu wake, japokuwa ulinichochea dhidi yake, nimwangamize pasipo sababu."
# Je umemwangalia mtumishi wangu Ayubu?
Hili swali la kejeli kwa kweli inatengeneza maelezo. Tafasiri kama katika 1: 6. "Angalia mtumishi wangu Ayubu."
# mtu mwenye haki na mkamilifu
Neno "haki" na "mkamilifu" yana maana sawa na yanaeleza kwamba Ayubu alikuwa muadilifu. "Alitenda yaliyo mema mbele za Mungu."
# mmoja aliye mcha Mungu na kuepukana na uovu.
Hapa uovu unazungumziwa kama vile eneo ambalo mtu ataepuka kwenda huko, badala ya kufanya matendo maovu. "alikataa kufanya uovu" (Tafasiri kama katika 1: 1)
# Hata sasa anashikamana na utimilifu wake
"amesalia amejitoa kikamilifu kufanya yale yaliyo ya haki na kweli"
# ulinichochea juu yake
"ulinishawishi bila sababu nimshambulie"
# nimwangamize
Hapa "angamiza" linawakilisha "kumfanya awe maskini." "kumfanya yeye awe mtu maskini"