sw_tn/isa/38/12.md

28 lines
1.1 KiB
Markdown
Raw Permalink Normal View History

2019-05-21 20:17:16 +00:00
# Maelezo yaJumla
Hezekia anaendelea maombi yake ya maandishi.
# Maisha yangu yameondolewa na kubebwa mbali na mimi kama hema la mchungaji
Hii inazungumzia jinsi Yahwe anamaliza uhai wa Hezekia kwa haraka kwa kulinganisha kwa jinsi mchungaji anavyotoa hema lake kutoka ardhini. "Yahwe amechukua uhai wangu kutoka kwangu haraka kama mchungaji anavyopanga hema lake na kulibeba mbali"
# Maisha yangu yameondolewa
Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "Yahwe amechukua uhai wangu"
# Nimekunjua maisha yangu kama mfumaji; unanikata kutoka katika kitanda cha mfumi
Hii inazungumzia Yahwe kumaliza uhai wa Hezekia haraka kwa kulinganisha na jinsi mfumaji hukata nguo yake kutoka katika kitanda cha mfumi na kukikunjua juu. "unamaliza uhai wangu haraka, kama mfumaji anavyokata nguo yake kutoka katika kitnda inapokamilika"
# unakata
Hapa "unakata" ni umoja na ina maana ya Mungu.
# kitanda cha mfumi
chombo kinachotumika kufuma uzi pamoja kutengeneza nguo.
# kama simba anavunja mifupa yangu yote
Hezekia anazungumza jinsi alivyo katika maumivu makala kwa kulinganisha kuwa na mwili wake kuraruriwa na simba. "maumivu yangu ni kana kwamba nimeraruliwa na simba"