sw_tn/isa/21/03.md

20 lines
707 B
Markdown
Raw Permalink Normal View History

2019-05-21 20:17:16 +00:00
# viuno vyangu vimejaa maumivu
Maono haya ambayo Isaya anayaona yanasumbua yanasababisha maumivu kwake. Hapa anaelezea maumivu na mkakamao katika sehemu ya kati ya mwili wake.
# maumivu kama maumivu ya mwanamke katika uchungu vimenikamata
Isaya analinganisha maumivu yake na maumivu ya mwanamke anayezaa. Hii inasisitiza maumivu makubwa anayosikia.
# nimeinama chini kwa kile nilichosikia
Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "Kile nilichosikia kimenisababisha kuinama chini kwa maumivu"
# nimesumbuliwa kwa kile nilichokiona
Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "Kile nilichoona kimenisumbua sana"
# Moyo wangu unadunda, ninatetemeka kwa hofu
"Moyo wangu unapiga haraka na ninatetemeka"