sw_tn/isa/08/14.md

32 lines
1.5 KiB
Markdown
Raw Permalink Normal View History

2019-05-21 20:17:16 +00:00
# Maelezo ya Jumla
Isaya anaendeleza nukuu isiyo moja kwa moja ya Yahwe ambayo ilianza katika 8:11. Inaweza kutafsiriwa kama nukuu ya moja kwa moja na Yahwe akizungumza katika mtu wa kwanza.
# Atakuwa mahali patakatifu
Neno "mahali patakatifu" ni sitiari kwa ajili ya Yahwe kuwaweka watu wake salama na kuwalinda. "Atawalinda watakapokwenda kwake"
# atakuwa jiwe la kupiga, na mwamba wa kujikwaa
Maneno "jiwe la kupiga" na "mwamba wa kujikwaa" yote ni sitiari kwa ajili ya Yahwe kudhuru watu wake. Baadhi wanatafsiri "kupiga" na "kujikwaa" kama "kujikwaa" na "kuanguka"; wengine wanatafsiri kama "kosa" na "kujikwaa". "atawadhuru watu wake, kama mwamba ambao watu hupiga miguu yao na kujikwaa, na kama mwamba ambao husababisha watu kuanguka"
# atakuwa mtego na kikwazo kwa watu wa Yerusalemu
Maneno "mtego" na "kikwazo" ina maana karibu na kitu kimoja na inasisitiza ya kwamba pale ambapo Yahwe ataamua kuadhibu watu wa Yerusalemu hawataweza kutoroka. "atawatega watu wa Yerusalemu ili wasiweze kumtoroka"
# mtego
chombo ambacho hukamata ndege katika wavu au kikapu
# kikwazo
mtego ambao hukamata na kushika mguu wa mnyama au pua
# Wengi watajikwaa juu yake na kuanguka na kuvunjika, na kutegwa na kukamatwa
Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "Watu wengi watajikwaa ju ya jiwe, na watakapoanguka hawatainuka. Na watu wengi watakanyaga katika mtego, na hawataweza kutoka"
# kutegwa na kukamatwa
Maneno haya mawili yana maana moja na yanasisitiza ya kwamba watashikwa katika mtego.