# Maelezo ya Jumla Isaya anaendeleza nukuu isiyo moja kwa moja ya Yahwe ambayo ilianza katika 8:11. Inaweza kutafsiriwa kama nukuu ya moja kwa moja na Yahwe akizungumza katika mtu wa kwanza. # Atakuwa mahali patakatifu Neno "mahali patakatifu" ni sitiari kwa ajili ya Yahwe kuwaweka watu wake salama na kuwalinda. "Atawalinda watakapokwenda kwake" # atakuwa jiwe la kupiga, na mwamba wa kujikwaa Maneno "jiwe la kupiga" na "mwamba wa kujikwaa" yote ni sitiari kwa ajili ya Yahwe kudhuru watu wake. Baadhi wanatafsiri "kupiga" na "kujikwaa" kama "kujikwaa" na "kuanguka"; wengine wanatafsiri kama "kosa" na "kujikwaa". "atawadhuru watu wake, kama mwamba ambao watu hupiga miguu yao na kujikwaa, na kama mwamba ambao husababisha watu kuanguka" # atakuwa mtego na kikwazo kwa watu wa Yerusalemu Maneno "mtego" na "kikwazo" ina maana karibu na kitu kimoja na inasisitiza ya kwamba pale ambapo Yahwe ataamua kuadhibu watu wa Yerusalemu hawataweza kutoroka. "atawatega watu wa Yerusalemu ili wasiweze kumtoroka" # mtego chombo ambacho hukamata ndege katika wavu au kikapu # kikwazo mtego ambao hukamata na kushika mguu wa mnyama au pua # Wengi watajikwaa juu yake na kuanguka na kuvunjika, na kutegwa na kukamatwa Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "Watu wengi watajikwaa ju ya jiwe, na watakapoanguka hawatainuka. Na watu wengi watakanyaga katika mtego, na hawataweza kutoka" # kutegwa na kukamatwa Maneno haya mawili yana maana moja na yanasisitiza ya kwamba watashikwa katika mtego.