# Efraimu atavunjwavunjwa na hatakuwa kundi la watu tena
Hapa "Efraimu" ina maana wote wa ufalme wa kaskazini wa Israeli. Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "jeshi litaangamiza Efraimu, na hapatakuwa tena na watu wa Israeli"
# mkuu wa Samaria ni mwana wa Remalia
Hii ina maana Peka ni mfalme wa Samaria na Israeli yote. "mfalme wa Samaria ni Peka, ambaye n mwanamume dhaifu"
# kama hautabaki imara katika imani, hakika hautabaki salama
Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "Ukiendelea kuamini ndani yangu, hakika utabaki salama"