forked from WA-Catalog/sw_tn
44 lines
1.4 KiB
Markdown
44 lines
1.4 KiB
Markdown
|
# Taarifa ya Jumla
|
||
|
|
||
|
Isaya anazungumza na watu wa Yuda katika mtindo wa shairi. Anaendelea kufafanua kile kitakachotokea katika siku ya Yahwe wa Majeshi.
|
||
|
|
||
|
# Kiburi cha mtu kitashushwa chini
|
||
|
|
||
|
Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "Atawashusha chini watu wenye kiburi" au "Atamuwaibisha kila mwanamume mwenye kiburi"
|
||
|
|
||
|
# Kiburi cha wanamume kitaanguka
|
||
|
|
||
|
Nomino dhahania "kiburi" inaweza kutafsiriwa kama kivumishi. "wale watu ambao wana kiburi na wataacha kuwa na kiburi"
|
||
|
|
||
|
# Yahwe pekee ayainuliwa
|
||
|
|
||
|
Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "watu watamsifu Yahwe tu"
|
||
|
|
||
|
# Hizo sanamu zitapita mbali kabisa
|
||
|
|
||
|
"Sanamu zote zitatoweka" au "Hapatakuwa na sanamu zaidi"
|
||
|
|
||
|
# Wanamume watakwenda ... kutoka kwa hofu kuu
|
||
|
|
||
|
Maana kamili ya kauli hii inaweza kuwekwa wazi. "Wanamume watakwenda .. kujificha kutoka kwa hofu kuu"
|
||
|
|
||
|
# mapango ya mawe
|
||
|
|
||
|
"mapango katika mawe". Haya ni mawe makubwa, sio mawe madogo ambayo yanaweza kushikiliwa katika mkono.
|
||
|
|
||
|
# kutoka kwa hofu kuu ya Yahwe, na kutoka kwa utukufu wa ukuu wake wa enzi
|
||
|
|
||
|
Hapa nomino dhahania "hofu kuu" inaweza kuelezwa na kitenzi "kuogofya". "kutoka kwa uwepo wa kuogofya wa Yahwe" au "Kutoka kwa Yahwe kwa sababu utamwogopa sana"
|
||
|
|
||
|
# kutoka kwa hofu kuu ya Yahwe
|
||
|
|
||
|
kwa sababu walikuwa wanamuogopa sana Yahwe
|
||
|
|
||
|
# kutoka kwa utukufu wa ufalme wake
|
||
|
|
||
|
Hapa neno "utukufu" kufafanua "ufalme". "uzuri ambao anao kama mfalme"
|
||
|
|
||
|
# atakapoinuka kuogofya dunia
|
||
|
|
||
|
"pale Yahwe atakapochukua hatua na kusababisha watu wa dunia kumuogopa sana"
|