sw_tn/isa/01/27.md

20 lines
953 B
Markdown
Raw Permalink Normal View History

2019-05-21 20:17:16 +00:00
# Taarifa ya Jumla
Isaya anazungumza maneno ya Yahwe kwa watu wa Yuda katika mtindo wa shairi.
# Sayuni itakombolewa kwa haki, na waliotubu kwa utakatifu
Hii inaweza kuwekwa katika hali ya kutenda. Maana kamili ya kauli hii inaweza kuwekwa wazi. Maana zawezekana kuwa 1) " Yahwe atakomboa Sayuni kwa sababu watu pale hufanya kilicho haki, na atawakomboa wale wanaotubu kwa sababu wanafanya kile ambacho Yahwe anasema ni sahihi" au 2) "Yahwe atakomboa Sayuni kwa sababu ana haki, na atakomboa wale wanaotubu kwa sababu ni mtakatifu"
# Sayuni
Huu ni mfano wa maneno wa "watu wanaoishi juu ya Mlima Sayuni".
# Waasi na wenye dhambi wakandamizwa pamoja
Hii inaweza kuwekwa katika hali ya kutenda. "Mungu ataangamiza wale ambao huasi na kutenda dhambi dhidi yake"
# wale wanaomuacha Yahwe watatoweka kabisa
Hii inaweza kuwekwa katika hali ya kutenda. "na Yahwe atawaondoa kabisa wale wanaogeuka kutoka kwake" au "na Yahwe atawaua wote wanaomkataa"