# Taarifa ya Jumla Isaya anazungumza maneno ya Yahwe kwa watu wa Yuda katika mtindo wa shairi. # Sayuni itakombolewa kwa haki, na waliotubu kwa utakatifu Hii inaweza kuwekwa katika hali ya kutenda. Maana kamili ya kauli hii inaweza kuwekwa wazi. Maana zawezekana kuwa 1) " Yahwe atakomboa Sayuni kwa sababu watu pale hufanya kilicho haki, na atawakomboa wale wanaotubu kwa sababu wanafanya kile ambacho Yahwe anasema ni sahihi" au 2) "Yahwe atakomboa Sayuni kwa sababu ana haki, na atakomboa wale wanaotubu kwa sababu ni mtakatifu" # Sayuni Huu ni mfano wa maneno wa "watu wanaoishi juu ya Mlima Sayuni". # Waasi na wenye dhambi wakandamizwa pamoja Hii inaweza kuwekwa katika hali ya kutenda. "Mungu ataangamiza wale ambao huasi na kutenda dhambi dhidi yake" # wale wanaomuacha Yahwe watatoweka kabisa Hii inaweza kuwekwa katika hali ya kutenda. "na Yahwe atawaondoa kabisa wale wanaogeuka kutoka kwake" au "na Yahwe atawaua wote wanaomkataa"