sw_tn/gen/47/29.md

40 lines
1.0 KiB
Markdown
Raw Permalink Normal View History

2019-05-21 20:17:16 +00:00
# Wakati wa kufa kwake Yakobo ulipokaribia
Hii inazungumzia juu ya muda kana kwamba inasafiri na kutua mahali. "Muda wa Israeli kufariki ulipokaribia"
# Ikiwa nimepata kibali machoni pako
Hapa "machoni" ina maana ya fikra na mawazo. "Kama nimepata kibali na wewe" au "Kama nimekufurahisha"
# sasa
Hii haimaanishi "katika kipindi hiki" lakini inatumika kuvuta nadhari kwa lengo muhimu linalofuata.
# nimepata kibali
Hii ina maana ya kwamba mtu amekubalika na mtu mwingine.
# weka mkono wako chini ya paja langu
Tendo hili ni ishara ya kufanya ahadi ya dhati.
# unionyeshe uaminifu na kweli
Nomino inayojitegemea ya "uaminifu"na "kweli" zinaweza kutafsiriwa kama vivumishi. "nitendee kwa namna ya uaminifu na kweli"
# Tafadhari usinizike Misri
Neno "tafadhali" linaongeza msisitizo kwa ombi lake.
# Nitakapolala na baba zangu
Hapa "kulala" ni njia ya upole ya kumaanisha kufa. "Nitakapokufa na kujiunga na wa familia yangu waliokufa kabla yangu"
# Niapie
"Niahidi" au "Fanya kiapo kwangu"
# akamwapia
"allimuahidi" au "alifanya kiapo kwake"