# Wakati wa kufa kwake Yakobo ulipokaribia Hii inazungumzia juu ya muda kana kwamba inasafiri na kutua mahali. "Muda wa Israeli kufariki ulipokaribia" # Ikiwa nimepata kibali machoni pako Hapa "machoni" ina maana ya fikra na mawazo. "Kama nimepata kibali na wewe" au "Kama nimekufurahisha" # sasa Hii haimaanishi "katika kipindi hiki" lakini inatumika kuvuta nadhari kwa lengo muhimu linalofuata. # nimepata kibali Hii ina maana ya kwamba mtu amekubalika na mtu mwingine. # weka mkono wako chini ya paja langu Tendo hili ni ishara ya kufanya ahadi ya dhati. # unionyeshe uaminifu na kweli Nomino inayojitegemea ya "uaminifu"na "kweli" zinaweza kutafsiriwa kama vivumishi. "nitendee kwa namna ya uaminifu na kweli" # Tafadhari usinizike Misri Neno "tafadhali" linaongeza msisitizo kwa ombi lake. # Nitakapolala na baba zangu Hapa "kulala" ni njia ya upole ya kumaanisha kufa. "Nitakapokufa na kujiunga na wa familia yangu waliokufa kabla yangu" # Niapie "Niahidi" au "Fanya kiapo kwangu" # akamwapia "allimuahidi" au "alifanya kiapo kwake"