sw_tn/gen/43/03.md

28 lines
1.0 KiB
Markdown
Raw Permalink Normal View History

2019-05-21 20:17:16 +00:00
# Yuda akamwambia
Hii ni nukuu ndani ya nukuu. Inaweza kuwekwa kama nukuu isiyo moja kwa moja. "alituonya ya kwamba hatutauona uso wake hadi tumlete ndugu yetu mdogo pamoja nasi"
# Yule mtu
Hii ina maana ya Yusufu, lakini ndugu hawakujua alikuwa Yusufu. Walimtaja kama "mtu" au "yule mtu, bwana wa nchi" kama katika 42:29.
# alituonya, "Hamtauona uso wangu ndugu yenu asipokuwa nanyi"
Hii ni nukuu ndani ya nukuu. Inaweza kuwekwa kama nukuu isiyo moja kwa moja. "alituonya ya kwamba hatutauona uso wake hadi tumlete ndugu yetu mdogo pamoja nasi"
# alituonya kwa ukali
"alikuwa na hali ya ukali alipotuonya, akisema"
# Hamtauona uso wangu
Yuda anatumia msemo huu mara mbili katika 43:3-5 kuweka msisitizo kwa baba yake ya kwamba hawawezi kurudi Misri bila Benyamni. Msemo "uso wangu" una maana ya yule mtu, ambaye ni Yusufu. "Hamtaniona"
# ndugu yenu awe nanyi
Yuda ana maana ya Benyamini, mtoto wa Raheli wa mwisho kabla yeye hajafa.
# hatutashuka
Ilikuwa kawaida kutumia msemo wa "kushuka" kuzungumzia safari ya Kaanani kwenda Misri.