sw_tn/gen/41/01.md

44 lines
1001 B
Markdown
Raw Permalink Normal View History

2019-05-21 20:17:16 +00:00
# Ikawa
Msemo huu unatumika hapa kuweka alama ya mwanzo wa sehemu mpya ya simulizi.
# mwishoni mwa miaka miwili mizima
Miaka miwili ilipita baada ya Yusufu kutafsiri kwa usahihi ndoto za mnyweshaji wa Farao na mwokaji, ambao walikuwa gerezani pamoja na Yusufu.
# Tazama, alikuwa amesimama
Neno "tazama" hapa linaweka alama ya mwanzo wa tukio jipya katika simulizi kuu.
# amesimama
"Farao alikuwa amesimama"
# Tazama
"Ghafla". Neno la "tazama" hapa linaonyesha ya kwamba Farao alishangazwa kwa kile alichokiona.
# wakupendeza na wanene
"wenye afya na wanene"
# wakajilisha katika nyasi
"walikuwa wakila nyasi kando kando ya mto"
# nyasi
nyasi ndefu, nyembamba ambazo huota katika maeneo ya unyevunyevu
# Tazama, ng'ombe wengine saba
Neno "tazama" hapa linaonyesha ya kwamba Farao alishangazwa tena kwa kile alichokiona.
# wasiopendeza na wamekondeana
"wagonjwa na wembamba"
# ukingoni mwa mto
"kando kando ya mto" au "kando ya mto". Hii ni sehemu ya juu ya ardhi pembeni mwa mto.