sw_tn/gen/09/01.md

28 lines
1.2 KiB
Markdown
Raw Permalink Normal View History

2019-05-21 20:17:16 +00:00
# Zaeni, mkaongezeke, na muijaze nchi
Hii ni baraka ya Mungu. Alimwambia Nuhu pamoja na familia yake kuzaliana wanadamu wengine kama wao, ili kwamba wawe wengi wa aina yao. Neno "mkaongezeke" linafafanua jinsi gani wanapaswa "kuzaana"
# Hofu na utisho wenu vitakuwa juu ya kila mnyama aliye hai ... na juu ya samaki wote wa baharini
Mwandishi anazungumzia hofu na utisho kana kwamba ni vitu vya mwili ambavyo vingeweza kuwa juu ya wanyama. "Kila mnyama hai ... na samaki wote wa baharini watakua na hofu kubwa sana juu yako"
# Hofu na utisho wenu
maneno "hofu" na "utisho" zina maana moja na husisitiza jinsi wanyama walivyokuwa wanaogopa binadamu. "Hofu ya utisho kwako" au "Hofu ya kutisha kwako"
# kila mnyama aliye hai juu ya nchi
Hili ni moja kati ya makundi manne ya wanyama ambayo mwandishi ameorodhesha, na sio ufupisho wa wanyama waliosalia atakaowataja hapo baadae
# ndege
Huu ni msemo wa jumla kwa vitu vinavyopaa. "wanyama warukao" au "vitu vinavyoruka"
# juu ya kila kitu kiendacho chini juu ya ardhi
Hii inajumuisha aina yote ya wanyama.
# Vimetolewa katika mikono yenu
Mkono ni lugha mbadala kwa mamlaka ambayo mkono ulikuwa nayo. Hii inaweza kuwa katika hali ya kutenda. "Vimetolewa katika mamlaka yako" au "Nimeviweka chini ya mamlaka yako"