sw_tn/gal/06/17.md

24 lines
1.0 KiB
Markdown
Raw Permalink Normal View History

2018-04-12 01:01:04 +00:00
# Tangu sasa
Hii inaweza kumaanisha "mwisho" au "kwa kuhitimisha barua hii"
# mtu yeyote asinitaabishe
Maana zinaweza kukubalika ni 1) Paulo anawaamuru Wagalatia wasimtaabishe "Ninawaamuru kwamba : "msinitaabishe" au 2)Paulo anawaambia Wagalatia kwamba anaagiza watu wote wasimtaabishe. "Ninamwamuru kila mmoja kwamba: usinitaabishe" au 3) Paulo anaeleza matakwa yake, "sitaki mtu yeyote anitaabishe"
# kunitesa mimi
Maana zinazokubalika ni 1) "kuniambia mambo haya" au 2) kunisababishia matatizo" au "kunipa kazi ngumu."
# maana nimebeba chapa za Yesu mwilini mwangu
"NIna makovuya vidonda katika mwili wangu kwa sababu ya huduma yangu kwa Yesu" au "Bado nina alama ya makovu katika mwili wangu kwasababu mimi ni mali ya Yesu"
# Neema ya Bwana wetu Yesu Kristo iwe na roho
"Ninaomba kwamba Bwana Yesu atakuwa mwema katika roho zenu"
# ndugu
Hapa neno 'ndugu' linamaanisha Wakristo, kwa kujumuisha wanaume na wanawake wote, kwa kuwa waumini wote ndani ya Kristo ni washirika wa familia moja, na Mungu ndiye Baba yao wa mbinguni.