sw_tn/1co/16/13.md

20 lines
1.1 KiB
Markdown
Raw Permalink Normal View History

2018-04-12 01:01:04 +00:00
# Muwe macho, simameni imara, mtende kama wanaume, muwe na nguvu
Paulo anawasisitiza Wakorintho kwa kuwapa maelekezo kana kwamba anatoa amri nne kwa askari wa vita. Hizi amri nne zinamaanisha jambo lilelile.
# Muwe macho
Paulo anawaambia watu watambue mambo yanayotokea kama vile walinzi wavyokaa macho wanapolinda mji au Shamba. kwa maneno mengine anasema "muwe makini sana kuhusu kwa yeyote mnayemwamini" au " jilindeni na hatari yoyote"
# simameni imara
Paulo anawahimiza waendelee kuamini katika Kristo kulingana na mafundisho yake, wawe kama askari wasiokubali kurudi nyuma wanaposhambuliwa na adui. hii inamaana: 1) " endeleeni kuamini kile tulichowafundisha" au 2) " endeleeni kumwamini Kristo kwa udhabiti wote"
# mtende kama wanaume
katika nyakati alizoishi Paulo na watu aliowaandikia barua yake, ilikuwa kawaida kwa wanaume kufanya kazi ngumu kwa ajili ya mahitaji ya familia na kupigana dhidi ya maadui. kwa uwazi zaidi inamaanisha " timizeni wajibu wenu"
# yote myafanyayo yafanyike katika upendo
"lazima kila jambo mnalolifanya lioneshe kuwa mnaupendo kwa watu"