sw_tn/1co/15/22.md

20 lines
886 B
Markdown
Raw Permalink Normal View History

2018-04-12 01:01:04 +00:00
# Adamu
Adamu alikuwa mtu wa kwanza ambaye aliumbwa na Mungu. Adamu na mke wake Eva waliumbwa katika sura ya Mungu. Mungu alimuumba Adamu kutoka katika mavumbi na kumpulizia pumzi ya uhai.
# Kifo, kufa
Maneno haya yametumika kumaanisha kifo cha kimwili na kifo cha kiroho. Kifo cha kimwili inamaanisha mwili wa mtu unapokoma kuwa na uhai. Kifo cha Kiroho, inamaanisha watenda dhambi wanapokuwa wametengwa na Mungu kwa sababu ya dhambi zao.
# Kristo
Neno Kristo au Masihi linamaanisha " aliyetiwa mafuta" na neno hili linamhusu Yesu, Mwana wa Mungu.
# Hai
Neno hili linamaanisha kuwa na uzima, iliyohai. Wakati mwingine linatumiwa kwa lugha ya picha kuelezea uzima wa kiroho.
# matunda ya kwanza
Neno"matunda ya kwanza" linamaana ya sehemu ya mazao,matunda au mboga zilizokuwa za kwanza kuvumwa wakati wa majira ya mavuno. Waisraeli walitoa matunda haya kama sadaka kwa Mungu.